Thursday, 4 August 2016

Abiria wa kike kutengwa na wanaume feri ya Mombasa

Abiria wakiingia katika Feri ya Likoni huko Mombasa Kenya
 Abiria wakiingia katika Feri ya Likoni huko Mombasa Kenya
Baraza la kaunti ya Mombasa nchini Kenya linapanga kuwatenga abiria wa kiume na wenzao wa kike katika kivuko cha likoni kufuatia visa vya unyanyasaji wa kingono katika kivuko hicho.
Baraza hilo tayari limezindua mpango huo kufuatia mapendekezo ambayo yameungwa mkono na serikali kuu pamoja na ile ya baraza hilo.
Tayari serikali ya Kenya imelipatia shirika la huduma za ferry katika kivuko hicho shilingi milioni 250 ili kuweka kamera za kuwachunguza wanaume hao wanaowanyanyasa wanawake pamoja na wahalifu wengine wanaoabiri feri hiyo.
Madiwani wa eneo hilo walichukua hatua hiyo kufuatia malalamishi kwamba wanawake huviziwa na baadaye kunyanyaswa kingono wakati feri hizo zinapojaa watu.
Wanaume kadhaa wamepatikana na hatia na kufungwa jela kwa kuwavizia na kuwashika abiria wawanawake.
Mtu mmoja anahudumia kifungo jela baada ya kupataikana na hatia ya kumnyanyasa mwanamke katika kivuko hicho.
Katika kisa chengine ,mtu mmoja alipigwa na abiria alipojaribu kumpiga busu mwanamke ndani ya feri hiyo.

No comments: