Thursday 4 August 2016

Ajifungua mtoto akiwa na miaka 63

Mama mzee zaidi nchini Australia akiwa na mchumbawake

  •  Mwanamke mwenye umri wa miaka 63 akiwa na mpenziwe mwenye umri wa miaka 78
Mwanamke mmoja kutoka Australia amejifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 63 .
Mama huyo mwenye mwenyeji wa mji wa Melbourne alifaulu kujibebea ujauzito huo baada ya kutumia teknolojia ya kisasa ya kuhamisha kiinitete au embryo.
Mama huyo amejaaliwa kujifungua mtoto wa kike baada ya kuchangiwa Kiini tete hicho.
Mtoto huyo anayeishi Tasmania alizaliwa kupitia njia ya upasuaji mjini Melbourne Agosti mosi.
Bibi huyo alikuwa amejaribu sana kupata mtoto kupitia teknolojia ya kupandikisha mimba au IVF lakini bila mafanikio.
Kiinitete kikiandaliwa kwa njia ya IVF
Kiinitete cha msichana huyo kilipandishwa ughaibuni
Hata hivyo mumewe mwenye umri wa miaka 78 hakufa moyo aliendelea kutafuta mbinu za kufanikisha ndoto yake ya kuwa mama siku moja.
Na siku hiyo iliwadia Agosti mosi.
Mama huyo na mwanaye wanaendelea kupata nafuu katika hospitali moja ya kibinafsi mjini Melbourne.
Kabla ya mafanikio ya mama huyo, mwanamke aliyekuwa anashikilia rekodi ya kupata mtoto akiwa na umri wa juu zaidi alikuwa na miaka 60.
Hata hivyo mwanamke anayeshikilia rekodi ya kuwa mzazi katika umri wa juu zaidi anatokea Romania.
Bibi huyo Adriana Iliescue alijifungua mwaka wa 2005 akiwa na umri wa miaka 66.
Vituo vya afya ya uzazi nchini Australia huwa vinakataa kupandisha wanake na ujauzito akiwa wamezidi umri wa miaka 53 na hiyo ndiyo iliyomlazimu mama huyo kupandishiwa ujauzito ugaibuni.





cHANZO: BBC

No comments: