Friday 11 November 2016

IJUE MAANA YA NDOTO YA KUJISAIDIA HAJA KUBWA UWAPO USINGIZINI

   


KITENDO CHA KUJISAIDIA HAJA KUBWA
Mara nyingi ndoto huja kama fumbo au mfano ili kuelewa maana ya ndoto ulio ota yakulazimu ufahamu nini maana ya fumbo au mfano ulio uwona katika ndoto.
Kuota kitendo cha karaha au kuudhi haimaanishi kua hiyo ndoto ni mbaya. Mfano kuota unajisaidia
haja kubwa au ndogo.

Wataalamu mbalimbali wa maswala ya ndoto na utabiri wamekuja na dondoo hizi kulingana na ndoto hizi ambazo mara nyingine si rahisi mtu kuziota hasa ndoto hii ya kuota unajisaidia haja kubwa

MAANA YA KUJISAIDIA

Kwanza ifahamike kua kujisaidia ni tendo la kushusha au kuondosha adhaa zilizo katika mwili, kwahiyo mwenye kuota anajisaidia hajakubwa au ndogo hii inamaanisha kua mtu huyo ameshusha au atashusha mambo yenye kumuhemeza hii inamaanisha kua mtu huyo ataondokewa na matatizo na mambo magumu alionayo.

NB: Tofauti kati ya haja kubwa na ndogo ni kwamba (1) Ukiota unajisaidia haja kubwa hii ina maanisha utaondokewa na Matatizo makubwa na madogo ulionayo.

(2) Ukiota unajisaidia haja ndogo inamaanisha utaondokewa na matatizo madogomadogo  tu ulionayo.

No comments: