Friday 20 May 2016

Ndege ya Misri yatoweka ikitoka Paris



Ndege
 Mwezi Machi ndege nyingine ililazimishwa kuelekea Cyprus

Ndege moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.
Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri. Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga.
Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.


CHANZO BBC

No comments: