Msemaji wa Serikali
ya Nigeria amesema msichana kutoka Chibok, aliyeokolewa hivi karibuni
kutoka mikononi mwa Wanamgambo wa Boko Haram, atakutana na Rais
Muhammadu Buhari na kupata msaada wa kuweza kuchangamana na jamii yake.
Aliachiwa huru akiwa na mtoto mchanga, hili ni tukio la uokoaji la kwanza kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili..
Zaidi ya wasichana mia mbili walitekwa na kundi hilo la Boko haram mwezi April mwaka 2014.
Jeshi
la Nigeria limesema tayari limeshamkamata mfuasi wa Boko Haram ambaye
inasemakana ni mume wa msichana huyo. Zaidi ya wasichana mia mbili
walitekwa na kundi hilo la Boko haram mwezi April mwaka 2014.
Msemaji
wa serikali ya Nigeria Garba Shehu amekiambia chanzo chetu kuwa msichana huyo wa
Chibok, aliyeokolewa hivi karibuni kutoka katika mikono Boko haramu
atakutana na Rais Muhammadu Buhari na atapewa msaada na serikali ili
aweze kurejea katika jamii.
Naye Aboku Gaji ambaye ni kiongozi wa
kikundi cha wanamgambo ambaye alimuokoa binti huyo na kukiambia chanzo chetu juu
ya namna familia yake ilivyompokea aliporudishwa nyumbani.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment