Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa
chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold
Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi
dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa Majeshi
Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.
Akiongelea tukio Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei, 17 mwaka huu majira ya saa 3 asubui.
Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi
kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya
nchi huku akuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.
“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya, Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti, hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo,“ alisema Mkumbo.
Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtuhumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yasemayo,
”Dk. Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba Mungu mauaji ya kisiasa
yaliyotokea Zanzibar yawe kwaviongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi
wa kawaida” hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijami.
yaliyotokea Zanzibar yawe kwaviongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi
wa kawaida” hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijami.
Mkumbo alisema
kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo
kamilika, huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii
kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratibu za
kisheria .
dwerj
No comments:
Post a Comment