Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari
na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa
mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini
kuanzia tarehe 01 - 05 Juni 2016.
Vijana
waliochaguliwa, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT
Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga –
Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT
Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.
Aidha,
wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities)
wanatakiwa kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani,
ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT
linawataka vijana hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za michezo kama
vile ‘track suit’, bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa
waliopangiwa kwenye makambi yenye baridi kama JKT Makutupora, JKT
Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT Mtabila.
Mkuu
wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kujiunga
na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, uhodari,
stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia
Taifa letu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 20 Mei 2016
No comments:
Post a Comment