Jeshi la Nigeria
limesema kuwa msichana mwingine aliyetekwa na wanamgambo wa Boko Haram
zaidi ya miaka miwili iliyopita kutoka shule ya Chibok ameokolewa.
Msemaji
wa Jeshi kanal S K Usman hakueleza kwa undani namna ambayo msichana
huyo ambayr hakutajwa jina aliokolewa,lakini akasema patakuwa na maelezo
zaidi baadae.
Siku ya Alhamisi msichana mwingine mwenye miaka 19
ambaye alifnikiwa kutoroka katika kambi ya Boko Haram, Amina Ali
Nkeki,alipelekwa katika mji mkuu Abuja akiwa na mtoto wake alizaliwa
wakati ametekwa, kwa ajili ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Muhammadu
Buhari.
Zaidi ya wasichana wengine mia mbili bado
hawajapatikana,huku ikidhaniwa kuwa bado wanashikiliwa katika misitu ya
Sambisa karibia na mpaka wa Cameroon.Gavana wa jimbo la Borno amesema
kwamba jeshi la nchi hiyo limejiandaa kuwakomboa wasichana hao.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment