Monday, 14 March 2016

AIBU YAKO AIBU YANGU!?

      AIBU YAKO AIBU YANGU!?

 

  Mnafumba macho nini, uchi huo tazameni,
Mwatuvalia vimini, tuone tuwatamani,
Mwavalia mapajani, tuone vilivyo ndani,
Twajiinamia chini, tusoona abadani.

Ubakaji mitaani, lawama kwetu za nini,
Hali mwavaa vimini, mnataka tutamani,
Mwapima kwanza nyumbani, na kudunda mitaani,
Wadogo zenu pembeni, waona na kutamani.

Twavuja jasho usoni, kutetea tamaduni,
Hamtaki kulikoni, vichwa vyenu vina nini,
Mwaiga vya ugenini, mmelishwa sumu gani,
Tumelalama acheni, mnakazana kwanini?

Enzi zile za zamani, walivaa magauni,
Marefu kwa kwenda chini, mapana kwenda pembeni,
Leo kimini pajani, eti mnasema fani,
Tunawafundisha nini, wana wetu masikini?

Kwetu watarithi nini, kiwafae maishani,
Au watarithi nini, tufanyacho cha thamani,
Kama sio ndo vimini, tuvaavyo bila soni,
Mnanesa mitaani, na kwenda navyo baani.

Haya maaadili gani, mnatukera jamani,
Mwaonyesha hadharani, twageukia pembeni,
Mwasema eti fasheni, mkome fasheni gani,
Hebu chaneni tupeni, vichomeni jalalani.

   Wengine surualini, wanadunda mitaani,
Zinazobana mwilini, wala hawaoni soni,
Waanikwa gazetini, aibu gani jamani?
Mwaaibika vueni, mkavae magauni!

Kaka zetu mitaani, mnatukera jamani,
Suruali viunoni, mnashusha chinichini,
Mnadunda mitaani, na mkono  mfukoni,
Hivi hamuoni soni, pandisheni suruali.

Mwavalia mapajani, tuone chupi za ndani,
Basi toeni mwilini, tupeni huko pembeni,
Yanini sasa mwilini, twaona vilivyo ndani.
Mnapita hadharani, wala hamuoni soni.

Mnaosuka kichwani, muache jama acheni,
Unayevaa heleni, dadako avae nini,
Unajidai fasheni, ujinga,fasheni gani?
   Ni jicho langu la tatu, liloona nikakerwa!

      

No comments: