Wednesday, 9 November 2016

Hizi hapa Siri za Ushindi waTrump

Ni wachache waliokuwa na fikra kuwa Trump angewania

Donald Trump alipita vizingiti vyote kutoka mwanzo wa kampeni yake ya kuwania urais zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Ni watu wachache walikuwa na fikra kuwa angeweza kuwania, lakini yeye alifanya hivyo. Walifikiri hangepata umaarufu lakini akafanya hivyo.
Wakasema hangeweza kushinda mchujo wowote lakini akafanya hivyo. Wakasema hangeweza kushinda uteuzi wa Republican lakini akafanya hivyo.
Image cop

ht
Majimbo yaliyokuwa ngome Democratic yalimpigia kura Trump
Kisha wakasema kuwa hakuna vile angeweza kushindana au hata kushinda na sasa ni yeye rais mteule wa Marekani.
Majimbo yaliyokuwa ngome ya Democratic yote yalimpigia kura Trump yakiwemo Ohio, Florida na North Carolina.
Watu wazungu walio na ajira hasa wale wasio na masomo ya chuo kikuu wanake kwa wamaume walikihama chama kwa wingi.
Donald Trump ni rais wa 45 wa MarekaniImage copyrigh
Image captionDonald Trump ni rais wa 45 wa Marekani
Wapiga kura wa mashambani walijitokeza kwa wingi huku Wamarekani wanaohisi kutengwa na watu wa mijini wakipiga kura kwa idadi kubwa.
Licha wa majimbo kama Virginia na Colorado kumchagua Clinton, jimbo la Wisconsin lilimwendea Trump na kusababisha matumaini ya Clinton kudidimia.
Trump alimdhalilisha John McCain. Akaanza ugomvi na mtangazaji wa kituo cha Fox News Megyn Kelly.
Wafuasi wengi wa Democratic walihamia RepublicanImage copyright
Image captionWafuasi wengi wa Democratic walihamia Republican
Aliomba msamaha shingo upande wakati kanda moja ya video ilitolewa, akijigamba jinsi alivyowadhalilisha kimapenzi wanawake.
Alipambana na pingamizi ndani ya chama chake na kushinda zote.
Trump alijenga himaya yake kutoka wa washindani wake kaiam mchujo. Wengie kama Marco Rubio, Ted Cruz, Chris Christie na Ben Carson baadaye walisalimu amri.
Hatimaye Trump anaelekea ikulu ya White HouseImage copyright
Image captionHatimaye Trump anaelekea ikulu ya White House
Wafuasi wengi wa chama akiwemo spika Paul Riyan na wengine, Trump hakuhitaji msaada wao, na kwa uhakika huenda ameshindana kwa sababu aliamua kuchukua msimamo dhidi yao.
Ni dalili ambayo wanasiasa wengine waliiona kwa mbali, Bernie Sanders na Tedd Cruz kwa mfano.
Lakini hata hivyo hakuna mtu aliyeilewa kama Trump mweyewe na ndivyo ikampeleka ikulu ya White House.

CHANZO: BBC

No comments: