Saturday, 15 October 2016

Wanaotumia Kope Bandia Hatarini Kupata Upofu wa Macho

Wanawake wanaotumia kope bandia wanahofiwa kuwa na hali ya hatari ya kupata upofu wa macho kutokana na gundi wanazotumiwa kutumia kope hizo kuripotiwa  kuwa na athari kwenye macho yao.

Tahadhari hiyo imetolewa na mratibu wa huduma ya macho ya mkoa wa Iringa, Dk George Kabona,alipokuwa akitoa tathmini ya huduma ya macho ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya afya ya macho duniani.

“Ningependelea wasipende kuzivaa kama fasheni ya kawaida,kwasababu zina madhara sana. Kwasababu hizo kope unabandika kwa kile kitu ambacho ile chemical ya kubandikia ndio huwa inaogopwa zaidi kuliko hata kope zenyewe. Ingekuwa labda unazibana na stapler hivi labda lakini kuna kitu unabandikia ile kitu ndio jicho halikitaki kama kinaendelea kukaa pale muda mrefu,”alisema Kabona.

“Pia hupelekea uoni hafifu. Pia linaweza likawapelekea watu shida ya kuona kwasababu uoni hafifu kuna ule mkali na uoni hafifu wa nafuu. Ukiwa ule mkali utakuletea shida kwenye shughuli zako za kila siku. Ukiwa katikati kama unaangalia TV, ukiwa unataka kumuona mtu unasogea maisha yanaweza yakaendelea. Lakini kuna ule mkali kabisa unakaribia na upofu unahitaji huduma.”

No comments: