Monday, 17 October 2016

DORIS MOLLEL FOUNDATION YAANZISHA CLUBS MASHULENI KUONGEZA UELEWA WA MASUALA YA WATOTO 'NJITI'


Ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na uelewa mpana wa masuala ya watoto njiti (prematurity babies), Taasisi ya Doris Mollel imeamua kuongeza ufahamu huo kwa kuanza kutembelea shule mbalimbali zilizopo jijini Dar es Salaam na kuunda vikundi vidogo vya kujitolea (Clubs).

Vikundi hivyo vilizinduliwa Oktoba 15, 2016 kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa anahimiza jamii kuwa na moyo wa kujitolea, hivyo basi kwa kupitia vikundi hivyo itasaidia kuongeza molari ya kujitolea kwa kizazi kijacho kuanzia wakiwa bado mashuleni.

Vilevile vikundi hivyo vitakuwa vinajadili masuala mbalimbali yanayohusu watoto njiti, maisha baada ya shule na mambo mengine mengi.

Baadhi ya shule zitakazokuwa na vikundi hivyo (Clubs) ni shule za sekondari za Al-Muntazir, Alpha, Msimbazi, Good Samaritan, Green Acres, IST, Mbezi High na Salma Kikwete.

Sherehe za uzinduzi wa clubs hizo zilifanyika katika shule ya sekondari ya Salma Kikwete, zikiwezeshwa na kampuni ya ASAS DIARES pamoja na Taasisi ya Rehema Friendship and Solidarity Trust ambao walitoa vitabu kwa ajili ya kuongeza ufahamu wa wanafunzi wa kile wanachofundishwa na walimu wao.
Mgeni rasmi alikuwa ni Bi. Anna Mgwira, waalikwa wengine ni pamoja na Bi. Doroth Kipeja, Bi.Lisa Jensen, wawakilishi kutoka shule tajwa pamoja na mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Bi. Doris Mollel akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Taasisi hiyo Bi. Rahma Amood.


No comments: