Mzozo umezuka nchini Pakistan kuhusu shamba
ambapo kiongozi wa zamani wa mtandao wa al-Qaeda Osama bin Laden alikuwa
anaishi mjini Abbottabad.Bin Laden aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani katika shamba hilo Mei 2011. Osama aliuawa Mei 2011
Maafisa wa jiji wanataka kugeuza shamba hilo kuwa uwanja wa kuchezea watoto. Hata hivyo, jeshi linataka kipande hicho cha ardhi kigeuzwe na kuwa makaburi.
Kuna
baadhi ya wakazi wanaotaka shamba hilo litumiwe kujenga shule ya
wasichana huku baadhi ya wanajeshi nao wakitaka ligeuzwe kuwa bustani ya
burudani na kutumiwa kuzalisha mapato kwa serikali.
Huku mzozo kuhusu pande hizo mbili ukiendelea, jeshi mnamo
Jumatano lilifika na kujenga ua, jambo lililoshangaza maafisa wa baraza
la jiji.
Bin Laden aliishi kwenye jumba la ghorofa tatu lililo
kwenye shamba hilo bila kujulikana kwa miaka kadha. Jumba hilo lilikuwa
limezungushwa ua mrefu. Shamba hilo, lenye ukubwa wa mita 3,530 mraba na linalokadiriwa kuwa
na thamani ya $285,000 (£218,000), limekuwa wazi tangu wakati huo.
Baada
ya kifo cha Bin Laden, shamba hilo lilikabidhiwa serikali ya jimbo la
Khyber Pakhtunkhwa (KP) pambayo ilibomoa jumba hilo pamoja na ua ili
kuzuia eneo hilo lisigeuzwe na wapiganaji wa kijihadi kuwa eneo
'takatifu'.
No comments:
Post a Comment