Wednesday 20 July 2016

Mzoga wa nyangumi wa tani 22 !


Image copyright
Image captionMzoga wa tani 22 wawashinda wenyeji kuuhamisha
Wakaazi wa California Marekani wamelazimika kuvumilia uvundo kutoka baharini kwa zaidi ya majuma matatu baada ya mzoga wa nyangumi mkubwa kusombwa na maji hadi ufukweni.
Mnyama huyo mkubwa wa baharini anakisiwa kuwa na uzani wa takriban tani 22.
Hakuna kifaa chochote kilichokuwa na uwezo wa kuhamisha mzoga huo.
Image copyright
Image captionHakuna kifaa chochote kilichokuwa na uwezo wa kuhamisha mzoga huo.
Tangu juni tarehe 30 alipopatikana ameaga ,Wally mwenye urefu wa mita 14 alionekana akielea baharini karibu na ufukwe wa Los Angeles.
Nyangumi huyo wa kike, alianza kuvunda na kusababishia wakaazi wa maeneo karibu na bahari wasijue la kufanya kutokana na ukubwa wake.
Wenyeji waliwaajiri wafanyikazi wa mijengo ambao walikuwa na trekta kubwakubwa za kunyanyua mawe na misumeno ya moto.
Image copyright
Image captionWenyewe hawakuwa na lingine ila kuvumilia harufu mbaya kwa majuma 3
Walimkata kata katika vipande vitatu lakini hata hivyo vilikuwa vizito mno kwa trekta za ujenzi.
Mwishowe waliagiza trekta kubwa zaidi yenye uwezo wa kunyanyua tani 10 ya mzoga huo unaovunda na kuibwaga baharini.
Wenyeji bado wanapata harufu mbaya majumbani mwao lakini wanaona kheri ikiwa mbali .

CHANZO: BBC

No comments: