Mke wa mgombea
urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donal Trump, Melania,
amefuta tovuti yake baada ya vyombo vya habari nchini Marekani kuanza
kutilia shaka ukweli wa baadhi ya madai yake.
Bi Trump amesema tovuti hiyo imefutwa kwa sababu haikuwa inaashiria wala kuonyesha mambo anayoangazia kwa sasa.Vyombo vya habari nchini Marekani vilikuwa vimetilia shaka ukweli wa madai kwamba ana shahada katika usanifu mijengo kutoka chuo kikuu kimoja nchini Slovenia, kama alivyokuwa ameandika katika wasifu wake mtandaoni.
Kitabu kuhusu maisha yake kilichochapishwa mwaka huu kinasema aliacha masomo baada ya mwaka mmoja kuangazia kazi ya uanamitindo.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment