Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Magonjwa Sita yatikisa nchi’
Gazeti la Jambo Leo limeripoti kuwa Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto imetaja magonjwa makuu sita; kuwa ndiyo yanayolisumbua taifa kwa sasa. Magonjwa hayo ni matatu ya kuambukiza, ambayo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamis Kigwangalla ni malaria, UKIMWI, kifua kikuu, kisukari, moyo na selimundu.
Kigwangalla aliyasema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hilo na kusema magonjwa hayo ni hatari yanapaswa kuchukuliwa hatuaza haraka na dharura kuyadhibiti kwani ndiyo yanayoongoza kwa vifo vya watu wengi zaidi ikilinganishwa na mengine.
No comments:
Post a Comment