Ni July 10, 2016 ambapo Tanzania imepata ugeni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ambae kupitia ujio wake
ameahidi kusaidia katika utekelezaji wa Miradi ya Maji Dar es Salaam na
Pwani, pia kusaidia kuendeleza sekta za Habari na Mawasiliano, Viwanda
vidogo vidogo na Vya kati, Kilimo, Afya na masuala ya Usalama nchini,
Ikulu Dar es Salaam.
Baada ya Waziri hiyo kutoa ahadi hizo
sasa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia kwenye ukurasa
wake wa instagram alisema….‘Imekuwa
siku ndefu ila yenye mafanikio makubwa sana kwa Taifa langu na
watanzania wote. Hongera sana Rais wetu, hongera pia Waziri Mkuu wa
India’- RC Paul Makonda
‘Karibu
tena Tanzania. Fursa zinazotafutwa na viongozi wetu naomba tuzitumie
tusiishie kulalamika tu. Sasa kilimo cha mazao jamii ya kunde soko lipo
tena la uhakika. kwa tani laki 1 tunaigiza dola Milioni 300, je kwa tani
Milioni 7 si itakuwa dola bilioni kadhaa. Vijana tuchangamke India
wanahitaji zaidi ya tani Milioni 7 ya mazao ya kunde,choroko na dengu- RC Paul Makonda
No comments:
Post a Comment