Friday, 3 June 2016

SAKATA LA UDOM: Je, ni kwel raisi JPM hapendi siasa?


Akitoa tamko la serikali Bungeni, Waziri mwenye dhamana ya Elimu Ndalichako alisema sakata la UDOM limetokana na mgomo wa wahadhiri kutolipwa fedha zao zinazofikia Milioni 800 wakati Mkaguzi wa ndani wa chuo anasema ni milioni 200 na kuwa serikali inashughulikia na wanafunzi wataitwa.

Mkuu wa nchi jana  yeye anasema WAMEWAFUKUZA wanafunzi kwa vile wale ni VILAZA wanaopewa tuu pesa za mkopo wakiwa hawastahili kusoma chuo kikuu na kuwa kama wengine wangegoma basi nao wangeenda. Hataki mchezo kabisa.

Hizi ni kauli mbili zinazokinzana ndani ya serikali moja. Hii inaleta picha gani kwani kwa vyovyote vile moja lazima ni ya kweli nyingine ni uongo. Kwa nini watu wazito hivi wakinzane katika kauli zinazohusu maisha ya Watanzania?



No comments: