Malawi imemfuta kocha wa timu ya taifa pamoja na msaidizi wake.
Mikataba ya Ernest Mtawali na msaidizi wake Nsanzurwimo Ramadahan, ilitarajiwa kumalizika 31 Julai.Wawili hao wamefutwa baada ya Malawi kuondolewa kutoka michuano ya Kombe la Cosafa katika hatua ya makundi.
Mtawali, 49, aliyekuwa kiungo wa kati wakati wa uchezaji wake, alichukua hatamu katika timu ya taifa Agosti 2015.
Chini ya uongozi wake, timu hiyo ya taifa ilishinda mechi sita, ikashindwa mechi sita na kutoka sare mechi nne.
Ramadahan hata hivyo anatarajiwa kurejea kama mkufunzi wa muda kuongoza Malawi dhidi ya Swaziland mwezi Septemba.
Mechi hiyo, itakayochezwa tarehe 3 Septemba mjini Blantyre, ndiyo ya mwisho kwa Malawi baada ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.
Matumaini ya Malawi kufuzu kwa michuano hiyo itakayoandaliwa nchini Gabon mwaka ujao mwezi Juni baada yao kulazwa na Zimbabwe mjini Harare. Malawi wanashika mkia Kundi L wakiwa na alama mbili.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment