Rais wa Korea
Kusini amesema nchi ya Uganda imeahidi kusitisha uhusiano wake wa
kijeshi na marafiki wake wa jadi Korea Kaskazini baada ya kuzuru mji
mkuu wa Kampala siku ya Jumapili, chombo cha habari cha AFP kimeripoti.
Korea Kaskazini imetuma wakufunzi wake wa kijeshi nchini Uganda kwa miaka tisa.Nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 1963 na rais Yoweri Museveni ametembelea nchi hiyo mara tatu, AFP imeongeza.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha vikwazo vikali kuwahi kutekelezwa kwa Korea kaskazini baada ya majaribio ya nuklia ya nne mwezi Januari.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment