Mabalozi wakereka sherehe ya Museveni
Bw. Museveni ameongoza Uganda tangu
1986
Wanabalozi kutoka nchi za Magharibi
waliondoka kwa hasira kutoka kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais Yoweri
Museveni siku ya Alhamisi.
Wanabalozi hao kutoka Marekani, nchi
za Ulaya na Canada waliondoka ghafla baada ya Bw Museveni kushutumu vikali
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani
imesema mabalozi hao pia walikerwa na kuwepo kwa Rais wa Sudan Omar al-Bashir
kwenye sherehe hiyo.
Bw Bashir anasakwa na mahakama ya
ICC kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya halaiki.
Sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw
Museveni, ya tano tangu achukue madaraka mwaka 1986, ilihudhuriwa na viongozi
kutoka Chad, Ethiopia, Kenya, Somalia, South Africa, South Sudan, Tanzania na
Zimbabwe.
Akihutubu, Bw Museveni alisema ICC
ni “kundi la watu bure” na akasema haiungi mkono tena.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa
Marekani Elizabeth Trudeau alisema: "Kutokana na kuwepo kwa Rais Bashir na
matamshi ya Rais Museveni, ujumbe wa Marekani, pamoja na wawakilishi kutoka
nchi za EU na Canada, waliondoka kutoka kwenye sherehe kuonyesha kutofurahishwa
kwao (na vitendo hivyo).”
Bw Bashir anasakwa na mahakama ya
ICC
"Tunaamini kwamba kuondoka
kwenye sherehe ndilo jibu sahihi kwa kiongozi wa nchi anayepuuzilia mbali
juhudi za kuhakikisha haki kwa waathiriwa wa mauaji ya halaiki, uhalifu wa
kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.”
Bi Trudeau alisema inashangaza zaidi
ikizingatiwa kwamba Uganda ni taifa mwanachama wa Mkataba wa Roma, mkataba
uliounda mahakama ya ICC.
Mahakama hiyo yenye makao yake mjini
The Hague, Uholanzi ilitoa vibali vya kukamatwa kwa Bw Bashir mwaka 2009 na
2010 kwa makosa ya mauaji ya halaiki yanayodaiwa kutekelezwa eneo la Darfur,
magharibi mwa Sudan.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment