Friday 11 November 2016

Zuckerberg awajibu wanaosema Facebook imemsaidia Trump kushinda uchaguzi

150817121249-trump-zuckerberg-immigration-540x304
Uchaguzi Mkuu wa Marekani umemalizika kwa Donald Trump kuibuka na ushindi na mambo mengi yakizidi kujitokeza ikiwa wakazi wa nchi hiyo kufanya maandamano ya kumpinga  Trump kuwa rais na mengine yakihusisha mtandao wa kijamii wa Facebook umehusika kusababisha Trump kuibuka na ushindi.
Habari hizo zimemfikia Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg na kuamua kuzungumza kuhusu tetesi hizo ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kusababisha mtandao huo kupoteza umaaruffu wake kwa kujihusisha na mambo ya kisiasa ambayo yanaweza kuchangia kuwagawa.
Zuckerberg amesema habari hizo sio za kweli na kuna watu wameamua tu kuzisambaza lakini Facebook haijahusika kwa namna yoyote kumfanyia mgombea yoyote kampeni ili ashinde.
“Hilo wazo la kuweka habari za uongo kuwa Facebook imeshawishi watu katika uchaguzi kwa namna yoyote ni wazo la hovyo sana,” alisema Zuckerberg wakati akizungumza katika mkutano wa unaohusu Teknolojia uliofanyika California, Marekani na kuongeza.
“Tuna kazi nyingi za kufanya, sitaki kulikuza hili jambo kutokana na umuhimu wake sababu uchaguzi unaweza kuwa na madhara kwa kila mtu katika nchi hii na hata kwa dunia nzima,

No comments: