Maelfu ya watu wanaopinga ushindi wa Donald Trump kwenye uchaguzi wa Urais, wameendelea kuandamana mtaani kwa usiku wa pili sasa katika miji mbalimbali nchini Marekani
.Waandamanaji wa huko Portland, Oregon, walikabiliana vikali na polisi. Kile kilichoanza kama maandamano ya amani ya watu zaidi ya 4,000, kimegeuka kuwa na fujo.
Watu hao wameharibu biashara, magari na kuwatupia vitu polisi. Maandamano mengine yanaendelea kwenye miji ya Los Angeles, Philadelphia, Denver, Minneapolis, Baltimore, Dallas na Oakland, California.
Rais huyo mteule, Trump ameyalaani maadamano hayo.
“Just had a very open and successful presidential election. Now professional protesters, incited by the media, are protesting. Very unfair,” aliandika kwenye Twitter.
No comments:
Post a Comment