Sunday, 13 November 2016

Donald Trump: “Sihitaji hata dola moja kwenye mshahara wangu nikiingia Ikulu”

“Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”, ni kauli ya Rais mteule Donald Trump baada ya kuulizwa kwamba atakuwa akiufanyia nini mshahara wa Dola laki nne (400,000 kwa mwaka) ambazo ni mshahara wa Rais wa Marekani anapokuwa Ikulu ya White House.
Kauli hii aliitoa Donald Trump mshindi wa kiti cha Urais nchini Marekani wakati akiwa kwenye kampeni zake September 17, 2015, huko Rochester, New Hampshire: “Kitu cha kwanza ninachotaka kuwaambia na nitakifanya kama nikichaguliwa kuwa Rais, Sitakuwa nikichukua mshahara, hata dola moja siihitaji, hicho sio kitu kikubwa kwangu.” – Donald Trump
Trump said in a Twitter Q & A session last September: 'As far as the salary is concerned — I won't take even one dollar. I am totally giving up my salary if I become president'
Kwa mujibu ripoti mpya zilizotolewa na jarida la watu maarufu duniani Forbes, limetaja utajiri wa Rais huyo mteule kuwa unafikia Dola Bilioni 3.7 za Marekani ambazo ni zaidi ya shilingi Trilioni 8 za Tanzania 
Donald Trump alisikika akisema kwamba alikuwa akijigharamia kwa fedha yake mwenyewe wakati wa kampeni zake, hivyo hatachukua mshahara wake zaidi ya kupokea vitu vidogo ambavyo ni vya lazima akiwa Rais.

No comments: