Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeupitisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 uliojadiliwa kwa siku mbili.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa mwenye furaha
Mswada huo uliwasilishwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kisha wabunge wakaanza kuujadili.
Ukurasa wa twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umetoa taarifa hii:
Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari, 2016.Muswada huo sasa unasubiri kusainiwa na Rais kuwa sheria kamili.
Mapema jana wakati wamajadiliano mbunge wa Kondoa ambaye alikuwa Waziri wa Habari katika serikali iliyopita, Mhe.Juma Nkamia alisema muswada huyo ukipitishwa na kuwa sheria utamaliza matatizo na kujenga heshima kwa waandishi wa habari.
Hata hivyo wabunge wa upinzani waliupinga muswada huyo kwa madai umempatia mamlaka makubwa waziri.
Picha chanzo Mwananchi
No comments:
Post a Comment