Saturday 1 October 2016

TANZIA: Msanii maarufu wa filamu afariki dunia

Muigizaji mkongwe wa filamu za Nollywood nchini Naijeria, Martins Njubuigbo a.k.a Elder Maya amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa ini kwa muda mrefu.

Muigizaji huyo ni maarufu sana kwa kuigiza kama Chifu wa kijiji au mganga wa kienyeji, na taarifa zinasema Elder Maya alifariki tarehe 30 mwezi huu wa Septemba, na taarifa hizo za kifo ziliwekwa kwa mara ya kwanza na msanii mwenzie wa huko huko Naijeria, Yomi Fabiyi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Nigerian actor Elder Maya is dead

No comments: