Kampuni kubwa ya kutengeza simu aina ya smartphone Samsung,imeroptiwa kusitisha utengezaji wa simu aina ya Galaxy Note 7 kufuatia madai kwamba simu mpya zilizotengezwa kuchyukua mahala pa zile zilizo na matatizo ya betri pia zina matatizo.
Vyombo vya habari vya Reuters na kile cha Yonhap kutoka Korea kusini vimewanukuu baadhi ya maafisa ambao hawakutajwa majina wakisema kuwa kampuni hiyo imesitisha kwa muda utengezaji wa simu hizo.
Samsung imeambia BBC inaimarisha utengezaji wa simu hizo ili kuhakikisha ubora na usalama wake.
Hatua hiyo inajiri baada ya kampuni mbili nchini Marekani kusitisha uuzaji wa simu hizo .
Samsung ilisema siku ya Jumatatu pia itazuia usafirishaji wa simu hizo katika maeneo tofauti duniani ili kuzifanyia ukaguzi.
Kampuni hiyo ya Korea Kusini ilizirudisha simu hizo mnamo mwezi Septemba na kuwahakikishia wateja wake mwezi uliopita kwamba simu zilizorekebishwa ziko salama.
Lakini kumekuwa na ripoti nyengine tofauti za simu zilizorekebishwa kutoa moshi.
No comments:
Post a Comment