Thursday 1 September 2016

KUPATWA KWA JUA RUJEWA MBEYA

RUJEWA MBEYA 

ELEWA MAAN YA KUPATA KWA JUA:  Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua vyote kwa pamoja vitakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua.
Matokeo ya kupatwa ni kupungua kwa jua hadi kutoonekana tena na kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.
Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia.

 Kivuli hicho hakifuniki Dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.

Kisayansi kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua. Miongoni mwa aina hizo ni #KupatwaKwaJuaKabisa ; hii jua linapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii huonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.




Wanasayansi wanaelezea kupatwa kwa jua kama tukio linalotokea na kuonekana katika namna tofauti tofauti mfano; ni kupatwa kwa jua kikamilifu hali ambayo hutokea pale miali ya jua inapotea kabisa katika eneo husika kwa kipindi kifupi. Hali hii inapotokea eneo husika linakosa kabisa mwanga wa jua na kuwa giza.

Aina ya pili ni kupatwa kwa jua kisehemu; hii hutokea wakati eneo kubwa linapopata upungufu wa mwanga wa jua hali ambayo hupungua kadiri mtu anavyokuwa mbali na kitovu cha mstari wa kupatwa kwa jua. 

Kiwango cha upungufu wa mwanga wa jua hutegemea umbali mtu alipo kutoka kwenye kitovu cha kivuli kamili.

Aina nyingine ni kupatwa kwa jua kipete; hali hii inapotokea mwezi huzuia mwanga wa jua kufika kwenye dunia kwa vile huweka duara la kivuli cha mwezi kwenye dunia na hivyo mwanga wa jua huonekana kama pete. 

Inatarajiwa kuwa aina hii ya kupatwa kwa jua ndiyo itakayojitokeza tarehe 1 Septemba 2016 katika baadhi ya maeneo ya Bara la Afrika. Kwa hapa nchini hali hiyo inatarajiwa kujitokeza katika sehemu kubwa ya maeneo ya mikoa ya Nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya kusini mwa nchi. Hata hivyo, watu katika maeneo mengine ya nchi yaliyokaribu na ukanda huo wanatarajiwa kuona kupatwa kwa jua kisehemu yaani upungufu wa mwanga wa jua kwa dakika kadhaa, imetabiriwa takriban kakika tatu (3). 

Jua linatarajiwa kupatwa wakati wa asubuhi kati ya saa tatu asubuhi na saa sita.

3. Athari zake kwa Hali ya Hewa.
Kwa ujumla hakuna athari zozote kubwa zinazotarajiwa kutokana na hali hiyo. Hata hivyo, upo uwezekano wa kupungua kwa viwango vya joto katika maeneo ambapo kupatwa kwa jua Kipete kutajitokeza. Kwa kuwa tukio hilo la kupatwa kwa jua huchukua muda wa dakika chache tu hali ya joto itapungua kwa haraka katika kipindi kifupi na baadae kuongezeka kurudi katika hali yake ya kawaida. Viwango vya kupungua kwa joto vitatofautiana kulingana na umbali kutoka eneo la kupatwa kwa jua

4. Upekee wa tukio la kupatwa kwa jua
Tukio hili hutokea au kujirudia mara chache sana katika eneo husika. 
Inakadiriwa kuwa inaweza kuchukua kati ya miaka 350 hadi 400 kwa hali hiyo kujitokeza tena katika eneo litakapotokea mwaka huu 2016. Hii ndio sababu kwa watu wa eneo husika na wanasayansi hili ni tukio la muhimu na kumbukumbu muhimu ya maisha.



  

No comments: