Kundi moja la
vijana waliojawa na ghadhabu na ambao walikuwa wamejihami na fimbo
waliwavamia raia wa Uchina wanaofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya
kisasa ya Treni nchini Kenya.
Wafanyikazi 14 wa China walijeruhiwa
wakati wa shambulio hilo katika eneo la Narok, takriban kikomita 200
kusini magharibi mwa mji wa Nairobi.Washambuliaji hao walidaiwa kulalamikia kampuni ya kujenga barabara na madaraja ya China kwa kutowapatia ajira za ujenzi wa reli hiyo.
Makumi ya maafisa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo huku mamlaka ikifanya mikutano ya dharura kwa lengo la kutuliza hali.
Kuna Takriban raia 4000 wa China wanaofanya kazi nchini Kenya hususan katika viwanda vya ujenzi pamoja na biashara za kuuza vifaa vya kielektroniki.
chanzo: bbc
No comments:
Post a Comment