Wednesday, 3 August 2016

Basi la kutagaa lazinduliwa China

Maelfu ya wachina walipigwa na butwaa basi la kipekee linaloendeshwa na umeme lilipofanyiwa majaribio katika mji wa Qinhuangdao, Kaskazini mwa mwa China

  • Amini usiamini hili ni basi la kipekee linaloruhusu magari kupitia chini yake
Basi la kipekee lenye urefu wa mita mbili juu linaloruhusu magari ya kibinafsi kupitia mvunguni mwake limefanyiwa majaribio katika mji waHebei kaskazini mwa Uchina.
Basi hilo linalopigiwa upatu kutatua kabisa tatizo la usafirishaji wa watu katika miji yenye idadi kubwa ya watu ama Transit Elevated Bus (TEB) limefanyiwa majaribio nchini China.
Basi hilo linaloendeshwa kwa umeme linauwezo wa kubeba zaidi ya watu 300 .
Basi hilo kubwa lina urefu wa mita 21 na upana wa futi 25 .
Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao mwezi Mei.
Abiria katika mji wa Qinhuangdao, ulioko jimbo la Hebei China wakifurahia usafiri wa siku za usoni wa Transit Elevated Bus TEB-1
 Ndani inanafasi kubwa mno inaweza hata kuwabeba abiria 300
Abiria wakijaribu kuabiri basi hilo la kipekee katika kituo maalum cha kuabiri mabasi hayo mjini Qinhuangdao
Basi moja la TEB linauwezo wa kubeba abiria wote katika mabasi 8 ya kawaida !
Majaribio ya basi hilo la kipekee yalifanyiwa katika barabara iliyofanyiwa ukarabati yenye urefu wa mita 300m.
Basi hilo linauwezo wa kuhudumu kwa kasi ya Kilomita 60 kwa kila saa.
Takriban mabasi hayo manne yanawezwa kuunganishwa na hivyo kuwa na dereva mmoja.
Basi la kipekee la Transit Elevated Bus TEB-1 likiwa barabarani mjini Qinhuangdao, China
 Hivi ndivyo inavyoonekana
''Mabasi haya ni ya kipekee na moja ya faida yake kuu ni uwezo wake wa kubeba abiria wengi sana 300 kwa kila basi, pia itaokoa sana nafasi barabarani'' alisema mhandisi mkuu katika mradi huo mpya wa usafiri Song Youzhou.
''Inahudumu kama vile treni za kisasa za umeme ila gharama ya kuwekeza kujenga njia na ukarabati barabarani ikiwemo ujenzi wa vituo maalum vya TEB ni 1/5 ''

No comments: