Sunday, 17 July 2016

'Waasi' 6,000 wamekamatwa Uturuki

Image copyrightREUTERS
Image captionMisako zaidi dhidi ya wanajeshi waasi Uturuki
Utawala nchini Uturuki umevamia kambi za kijeshi kote nchini kuwatafuta wanajeshi wanaoshukiwa kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyozimwa siku ya Ijumaa.
Kambi za kijeshi zimevamiwa na kusakwa.
Katika oparesheni kwenye mji ulio magharibi wa Denizli saa chacha zilizopita kamanda mmoja wa kikosi cha jeshi na zaidi ya wanajeshi 50 walikamatwa.
Image copyrightREUTERS
Image captionMaelfu ya wanajeshi wamekamatwa.
Maelfu ya wanajeshi wamekamatwa.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini amesema kuwa jeshi limerejesha udhibiti katika asilimia kubwa ya kambi za kijeshi japo kuna baadhi ambazo zipochini ya usimamizi ya wale walionga mkono mapinduzi.
Majaji takriban 3000 ambao wanatuhumiwa kupinga serikali ya rais Reccep Teyyip Erdogan wamesimamishwa kazi.
Image copyrightGETTY
Image captionRais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema kuwa bunge litaamua ikiwa litabuni sheria ya hukumu ya kifo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema kuwa bunge litaamua ikiwa litabuni sheria ya hukumu ya kifo.
Wale waliokamatwa wanatajwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa kidini raia wa Uturuki anayeishi nchini Marekani Fethullah Gulen ambaye analaumiwa kwa kupamnga mapinduzi hayo.


CHANZO; BBC

No comments: