Mojawapo wa mwanamuziki mashuhuri mkongomani
Koffi Olomide,amejipata matatani baada ya kunaswa kwenye kamera akimpiga
teke mwanamke, anayesadikiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake.Tukio
hilo lilirekodiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ambako
alikuwa amewasili kwa tamasha lilopangwa kufanyika nchini Kenya. Wengi wa Wakenya wamekashifu vikali kitendo hicho
huku maoni katika mitandao ya kijamii yakitoa wito watu kutohudhuria
tamasha hilo na badala yake wakitaka akamatwe.
Wengine kupitia kitambulisha mada #KickKoffiOlomideBackToCongo kwenye Twitter wanapendekeza afurushwe kutoka Kenya.
Kwa upande wake Koffi Olomide, kwenye ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, amesema tukio hilo lilieleweka vibaya.
Amesema
alikuwa anajaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa
kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao
wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.
Katika video hiyo msichana huyo mchezaji anaonekana kukubaliana naye.
No comments:
Post a Comment