Friday 24 June 2016

Uingereza wapiga kura kujitoa katika umoja wa Ulaya

Yakiwa yamebaki majimbo matano Kati ya 382 kutangazwa, Uingereza wamepiga Kura kujitoa katika umoja wa ulaya baada ya miaka 48.
Waliopiga Kura kujitoa wameshinda kwa zaidi ya Kura milioni moja na laki moja. Sawa Na asilimia 52.
Wakati huo huo,Scotland ambao walipiga Kura ya kutaka kujitenga na Uingereza imesema matokeo ya Kura yameonesha wazi kuwa Scotland haina maisha ndani ya UK Bali wanataka kuishi ndani ya umoja wa ulaya.
Asilimia 63% ya waScotland walipiga Kura kubakia.
Pound imeshuka kwa kiwango kikubwa tokea matokeo kutangazwa baada ya kupanda kwa muda Tu wakati matokeo yaliyoonesha waliotaka kubakia wanaongoza.

No comments: