Saturday, 4 June 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, PIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA LUO ZHIJUN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 4,2016

1


2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam.
3 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga mara baada ya tukio la uapisho kukamilika.
5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun kutoka jimbo la Jiangsu nchini China.
6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun kutoka jimbo la Jiangsu nchini China, ikulu jijini Dar es Salaam.
7 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini lu youqing aliyeambatana na Kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China, Ikulu jijini Dar es Salaam.
8 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
9 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun kutoka jimbo la Jiangsu nchini China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam
10Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun pamoja na Balozi wa China hapa nchini lu youqing mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda.



CHANZO: Blog Rasmi Ya Raisi

No comments: