Monday 27 June 2016

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ITAANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 2016/2017 LEO TAREHE 27/JUNI HADI 31 JULAI 2016

http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2016/03/HESLB-Logo.png

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa taarifa kwa Umma na wadau wake wote kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya Mikopo kwa mwaka wa masomo 2016 /2017 kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31 Julai 2016.
Aidha bodi hiyo inawataka  waombaji wa mikopo watarajiwa wanapaswa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku (GUIDELINES AND CRITERIA FOR ISSUANCE OF STUDENTS’ LOANS AND GRANTS FOR THE 2016/2017 ACADEMIC YEAR) uliopo kwenye tovuti  ya Bodi ili kufahamu sifa za mwombaji na taratibu kufuata kabla ya kuomba mikopo kwa njia ya mtandao.
Utoaji wa Mikopo unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Na. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) hususani vifungu vyake vya 16 na 17.
Kwa taarifa hii, waombaji wote wa mikopo wanatakiwa kusoma mwongozo huo kabla ya kujaza maombi ya mikopo na wazingatie kuwa tarehe ya mwisho ya kuomba mikopo ni Julai 31, 2016.

No comments: