- hapa ni mkusanyiko wa picha kutoka matukio muhimu barani Afrika wiki hii, kuanzia michezo hadi maadhimisho ya miaka 25 tangu Somaliland ijitangazie uhuru.
- Jumanne, katika jiji la Nairobi, msichana anabeba mwanasesere kutoka kwa jumba ambalo limepangiwa kubomolewa. Serikali inabomoa nyumba zisizo salama baada ya jumba moja kuporomoka na kuua watu takriban 50 mwezi Aprili.
- Mnamo Ijumaa, mwanamke wa jamii ya Berber, Morocco anashiriki mashindano ya urembo ya Miss Rose katika mji wa Kelat, chini ya milima ya Atlas.
- Siku iliyofuata, katika bohari kubwa lililo karibu, mwanamke anatenganisha maua ya waridi kutoka shamba la Damask. Maua hayo hutumiwa kutengeneza bidhaa za urembo.
- Jumanne, wachezaji wa mpira wa vikapu wakiwa kwenye magurudumu, wanafanya mazoezi mjini Juba, Sudan Kusini. Wengi waliumia wakati wa vita vya kupigania uhuru wa taifa hilo kutoka Sudan.
- Nchini Afrika Kusini siku ya Ijumaa, JP "Tinkerbell" Kruger (kushoto) na Yannick "Black Mamba" Bahati (kulia) wapigana katika pambano la ubingwa Ijumaa.
- Siku iliyofuata, nchini Ivory Coast, mvuvi aandaa nyavu zake kwenda kuvua samaki. Wavuvi wa kawaida wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa wavuvi wanaotumia vifaa vya kisasa.
- Jumatano, jimbo la Somaliland liliadhimisha miaka 25 tangu lijitangazie uhuru wake kwa gwaride katika mji mkuu Hargeisa. Jimbo hilo halijatambuliwa na jamii ya kimataifa kama nchi huru.
- Siku iyo hiyo, mjini Abuja, Nigeria, raia waliandamana kupinga kupanda kwa bei ya mafuta kwa 67%.
- Jumatano, makundi ya kidini yaliandamana mjini Harare, Zimbabwe kupinga walichosema ni hatua za kupinga Ukristo katika shule zikiwemo kula kiapo cha kutumikia taifa. Walisema hatua hizo zinaenda kinyume na mafundisho ya Biblia.
- Jumatatu, wavulana hawa nchini Misri walijitosa majini kujaribu kuepuka joto kali mjini Cairo.
- Wachuuzi hawa wa tikitimaji katika mji wa Beghazi, Libya nao walijaribu kuwavutia wateja siku ya Jumapili.
- Polisi nchini Kenya nao walitumia nguvu kutawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga viongozi wa tume ya taifa ya uchaguzi. Baadhi ya mashirika baadaye yalisema walitumia nguvu kupita kiasi..
No comments:
Post a Comment